Kunihusu

Picha yangu
Teacher, comedian and event master of ceremonies.

Ijumaa, 29 Desemba 2017

LISTI YA WASANII 10 WALIOFANYA VIZURI MWAKA 2017

HII NI LISTI YA WASANII 10 KUTOKA TANZANIA WALIOFANYA POA SANA MWAKA 2017.

Na, Erasto The Ninja.

Yakiwa yamesalia masaa machache sana kuweza kuukamilisha mwaka huu basi ingekuwa ni vizuri zaidi kama ningetaja wasanii 10 bora ambao wameweza kufanya poa sana mwaka 2017. Karibu twende pamoja.

1. ASLAY
Akiwa ni moja kati ya vijana waliotoka kupitia mgongo wa lebel ya Mkubwa na Wanawe kutoka Temeke basi Aslay amekuwa ni moja kati ya vijana ambao wamefanya poa sana mwaka huu. Hakuna wa kupinga kuwa kona zote za mitaa ya hapa nchni Tanzania ulikuwa huwezi kupita bila kusikia wimbo wa Aslay ukichezwa. Akiwa amefanya kazi zake kwa Shirko producer wa Moja Moja Records lakini pia Aslay alifanya hit kali pia kutoka kwa producer Zest. Nyimbo zake kali alizotoa mwaka huu ni kama Natamba, Baby, Pusha na nyimbo kibao tu ambazo siwezi kuzitaja zote.

2. NANDY.
Ni product kutoka Tanzania House of Talent ambapo baadhi ya wasanii kama Barnaba, Amin, Rachel, Beka na Lameck Dotto walipitia hapo. Kuna watu husema kuwa Nandy ndio amekuwa mrithi wa Ruby hasa kwa nyimbo zake kali na jinsi anavyoweza kutumia sauti yake vizuri. Nandy ndiye msanii wa kike ambaye kwa mtazamo wangu ndio kafanya vizuri zaidi mwaka huu.

3. DIAMOND PLATNUMZ.
Kiuhalisia mimi ni Team Kiba ila kwenye kitu kizuri siwezi kusema uongo. Diamond kafanya vizuri sana kwa hit zake alizotoa mwaka huu akiwa pamoja na team yake ya WCB. Diamond amefanya kazi na wasanii wakubwa kama Morgan, Patoranking na  The Big Boss *Rick Ross* kutoka USA. Chini ya Producer Laizer jua kuwa Diamond kafanya ngoma kali kama Sikomi, Love you die na ngoma kibao zingine.

4. ALI  KIBA.
Ni kijana kutoka Kariakoo Dar es Salaam aliyekuja kutambulika zaidi mwaka 2007 na wimbo wake wa Cinderella aliofanya pale *G. Record* chini ya producer *KGT*. Japo hakuwa na nyimbo nyingi ila hakuna wa kubisha kuwa "Seduce Me" no wimbo wa Kiba ambao ulikuwa gumzo sana nchini Tanzania hasa baada ya kuvunja record ya Vevo Afrika Mashariki. Ali Kiba amepata shoo nyingi sana hasa baada ya kutoa wimbo wa Seduce me uliofanyika kwenye studio za Man Walter (Combination Sound).

5. WEUSI.
Nashindwa nimtaje nani aingie kwenye list hii ila kwasababu wote hufanya kazi kwa ushirikiano basi sina budi kuwaweka hapa. Sio Joh Makini, G. Nako wala Nikki wa Pili ambaye unaweza kutia shaka kwenye kazi aliyoifanya kwenye tasnia ya muziki mwaka huu. 

6. VANESSA MDEE.
Moja kati ya wadau ambao husemekana kuwa wana uwezo mkubwa sana wa kutema kimombo basi Vanessa kafanya vizuri sana mwaka huu. Moja kati ya nyimbo alizotoa ni "Mapenzi ya Kisela" akiwa na "Mr. P" wa kundi la "P-Square" kutoka Nigeria. Vanessa Mdee pia kafanya collabo kibao za kimataifa na ndani ya bongo.

7. ZAIID.
Hakuna ngoma iliyopata gumzo bongo kama ngoma ya Zaiid "Wowowo" ambayo imefanya poa sana kwenye vituo vya radio na Tv hapa nchini Tanzania. Zaiid alikuwa kama ni msanii mpya kwenye game la muziki hasa kwa baadhi ya watu lakini ukweli ni kwamba Zaiid ni msanii ambaye alikuwa na nyimbo nyingi tu hata kabla ya wimbo wa  "Wowowo".

8. ROSTAM.
Ni kundi ambalo lilianza kama mzaha ila mwisho likawa official. Roma Mkatoliki kutoka Tanga na  Stamina kutoka Morogoro ni vijana wawili walioweza kufanya poa sana hasa na wimbo wao wa Hivi ama vile na Kibamia zilizofanyika pale Kiri Record kwa Producer Don.

9. ______________

10. _____________

Nimeacha wazi hapo namba 9 na 10 ili nawewe uweke wasanii wako wawili kukamilisha list hiyo.

Jumanne, 12 Septemba 2017

TUJIKUMBUSHE KIDOGO JUU 2PAC.


Leo Septemba 13 ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyewahi   kuwa nyota mkubwa sana kwenye miondoko ya Hip Hop namzungumzia 2pac Shakur a.k.a Makaveli. Ni msanii aliyezaliwa mwaka 1971 East Harlen-New York nchini Marekani na alianza kazi ya muziki mwaka 1987 akiwa kwenye kundi la Digital Underground. 
Mbali na kuwa mwanamuziki 2Pac alikuwa ni muigizaji na aliwahi kucheza muvi 6 akiwa kama starring na moja kati ya filamu aliyowahi kutoa ni Gang Related ya mwaka 1993. Hadi mauti yanamkuta 2Pac Shakur alikuwa amewekeza vizuri kwenye albamu maana aliacha albamu 5. Moja kati ya albamu zake ni All eyes on me, Strictly 4 Maniggaz na 7 Day theory (Don Kiluminant).

2Pac Shakur aliwahi kushirikiana na wasanii kama Nate Dogg, Snoop Dog, Rich Richie na The Notorious B.I.G. Amewahi kuwa kwenye kundi la Thug Life na lebo ya Interscope mwaka 1991-1995 kisha lebo ya Death Row mwaka 1995-1996.

2Pac  Shakur alifariki dunia majira ya saa 10 jioni Septemba 13 mwaka 1996 ikiwa ni siku 6 tangu kutokea kwa shambulizi lake. Usiku wa tarehe 7 septemba 1996 wakati Pac akitokea kwenye mpambano wa masumbwi kati ya rafiki yake Mike Tyson dhidi ya Bruce Ledon kwenye barabara ya Flamingo ndipo alipovamiwa na watu wasiojulikana wakiwa kwenye gari na kufanikiwa kumchapa risasi 4 na moja kati hizo risasi ilipiga pafu lake la kulia. Baada ya shambulio hilo  2Pac Shakur alikimbizwa kwenye hospitali ya University Medical Centre of Sourthen Nevada ambako ndiko mauti yalimkuta. Mtu aliyefanya shambulio lile hakuwahi kujulikana hadi leo japo kuna watu wengi sana walihusishwa na tukio hilo kama vile hasimu wake wa wakati huo B.I.G na Anderson.

Tutamkumbuka sana 2Pac Shakur kwa uwezo wake mkubwa wa kufanya muziki wa Hip Hop. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu 2Pac mahali pema peponi, Amina.

Imeletwa kwenu na Erasto The Ninja
Tel: 0768801115

Jumatano, 7 Juni 2017

KUWA WA KWANZA KUPATA TAARIFA NA BURUDANI KUPITIA BLOG HII.

Sasa ninjamedialive itakuwa ikikupa taarifa mbalimbali za burudani, siasa, uchumi na jamii popote pale ulipo. Tafadhali tembelea ukurasa huu ili uwe unapata taarifa zote uzipendazo.

 

MJANJA HAPITWI NA KITU.



Jumanne, 2 Mei 2017

MASHABIKI WA KR GENK WAZIDI KUONESHA LOVE KWA SAMATTA.

Jina la nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta limeendelea kuchukua headlines kutokana na kuonesha mchango katika timu hiyo.

Moja kati ya kitu ambacho kinatafsiriwa kuwa ni heshima na sifa kubwa kwa shabiki wa soka hususani barani Ulaya ni kupata jezi ya mchezaji anayempenda akiwa kaipata moja kwa moja kutoka kwa mchezaji husika iwe imesainiwa au katoka kuchezea mechi.

Samatta ameonekana kukubalika na mashabiki wa soka Ubelgiji kiasi cha shabiki kuingia na bango uwanjani akiwa kaandika “Samatta naweza kupata jezi yako tafadhali.?

MAMBO AMBAYO YAWEZEKANA YANAWEZA KUKUSHANGAZA ZAIDI DUNIANI.


Kila mwanasayansi duniani hutaka kugundua teknolojia flani ili kujijengea heshima na jina katika fani yake, lakini kuna baadhi ya vifaa vya kiteknolojia ambavyo vimegunduliwa na wanasayansi mbalimbali duniani ambavyo vimeleta gumzo na kushangaza watu wengi.

Leo May 2, 2017 nimeona si vibaya nikikusogezea teknolojia saba za kushangaza na kustaajabisha zilizowahi kutengenezwa na wanasayansi mbalimbali duniani.

1: Kiatu chenye kiyoyozi

Hii ni moja ya teknolojia ambayo ilistajabisha watu wengi baada ya kampuni ya Hydro-Tech kutengeneza kiatu ambacho kina kiyoyozi kinachosaidia mvaaji wa viatu hivyo kupata ubaridi akiwa sehemu zenye joto kali.kiatu hiki kinauzwa dola 75.




2: Jacket unayoweza kufanya kama TV

Mwaka 2015 kampuni ya Lenovo ilizinduwa jacket inayojulikana kama “screen jacket” ambayo unaweza kuigeuza na kuifanya Tv ambayo unaweza  kuangalia vipindi mbambali. ,jacket hili pia limewekewa program kama Netflix ambapo mtu anaweza kuangalia movie.
 .



3: Kifaa cha kupoozea chakula

Kifaa hiki cha kupoozea chakula cha moto kilitengezwa na kampuni Tech E kutoka Japan, Lengo la designer aliyekibuni kifaa hichi ni kusaidia kupoza chakula cha moto hasa kwa watoto.




4: Kifaa cha kuangalia movie huku unatembea

Kifaa hiki chenye muundo wa kofia kimebuniwa na kampuni ya B-tech kwa ajili ya watu wanaopenda kuangalia movie peke yao bila bughudha ,kifaa hiki kilipata umaarufu mkubwa mwaka 2015 na kiliuzwa zaidi ya pisi milioni 5 duniani kote.




5: Kifaa cha kukupa ulinzi

Mwaka 2016 kampuni ya Techstars ilizindua kifaa maalum ambacho kinaweza kutuma taarifa kwa familia na marafiki  iwapo mvaaji amepatwa na tatizo kwani itaonesha mahali alipo, Kifaa hiki kilibuniwa mahususi kwa ajili ya Wanawake wanapopata matatizo hasa ya kuvamiwa na kubakwa.





6: Kiatu kinachotumia bluetooth

Kampuni ya HSG-IMIT ilizindua kiatu kinachojulikana kama “smart shoes” kwa mara kwanza mwaka 2016 katika maonyesho ya  Consumer Electronics, kiatu hiki kinauwezo wa kuunganishwa na bluetooth ya simu yako ambapo unaweza kufunga na kufungua mikanda ya viatu kwa kutumia smart phone yako.




7: Mkanda wa kuzuia unene

Mwaka 2016 kampuni ya Samsung ilizindua mkanda maalum ambao mtu akiuvaa unamsaidia kujua ale chakula kiasi gani ili asinenepe, mtumiaji wa mkanda huu anaweza kuufunga na kufungua kwa kutumia simu yake ya mkononi.



Alhamisi, 27 Aprili 2017

TAZAMA ROBOTI INAYOWEZA KUPAMBANA NA WAHALIFU.





Ubunifu ndio unaiendesha dunia lakini sio kila mtu amepewa uwezo wa kubuni bali wapo wachache kwenye kundi la wengi ambao wana uwezo wa kubuni mambo mbalimbali ndiyo maana nimekuletea stori hii ya ubunifu wa hali ya juu.

Kampuni ya Silicon Valley imebuni mbinu mpya ya kupambana na uhalifu katika maduka makubwa baada ya kutengeneza robot ambayo kazi yake ni kupambana na uhalifu katika maduka makubwa zikitengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu ambapo zitafanya kazi bila usimamizi wa binadam na kukodishwa kwa Dollar 7 (£5) ambazo ni sawa Tsh. 15,400 kwa saa.

Katika stori hii iliyochapishwa na mtandao wa Daily Mail April 27, 2017 ni kwamba robot inayoitwa Knightscope K5 ina urefu wa futi 5 ni maalum kufanya patrol katika maduka makubwa, viwanja vya michezo na kumbi za cinema kwa lengo la kuhakikisha usalama wa maeneo hayo.

Lengo kuu la kampuni hiyo ni kuzalisha maroboti wengi zaidi ambao watasambazwa duniani kote wakikusudia kupunguza uhalifu hadi 50% ambapo kwa mujibu wa ripoti ni kuwa wanakusudia siku moja zitumike na Polisi katika kusaidia kupambana na uhalifu.

Mmoja wa watengenezaji wa Knightscope Stacy Dean Stephens alisema: “Tunaanza na maeneo ya umma, hivyo tunaziruhusu kufanya patrol kwenye maeneo kama maduka makubwa, kampasi, viwanja vya michezo na nyumba za cinema.”

Jumatatu, 17 Aprili 2017

MAGAZETI  YA LEO TAREHE 18 Aprili  2017















Source: Millardayo.com

L

RAIS MAGUFULI AITAKA TCU IWAACHIE WANAFUNZI WACHAGUE VYUO WANAVYOVITAKA.

Rais John Magufuli ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutowachagulia vyuo wanafunzi wa elimu ya juu na kuwaacha wanafunzi hao kuchagua vyuo wanavyovitaka wenyewe.




Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais Magufuli alipokuwa akizindua mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo alikitaka chuo hicho pia kutoza Sh 500 kwa siku tofauti na Sh 800 ambazo zinatoswa kwa hosteli nyingine.

“Ninaamini kama wanafunzi wangepewa nafasi ya kuchagua vyuo wanavyovipenda wenyewe, vyuo vya Serikali kama vile Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo Kikuu cha Mzumbe vingekuwa na wanafunzi wengi sana,” alisema Magufuli.

Aliendelea kwa kusema kuwa TCU imekuwa ikiwachagulia wanafunzi vyuo visivyo na sifa na makazi ya wanafunzi hivyo kusababisha wanafunzi hao kusoma katika mazingira magumu na wanapomaliza masomo yao hukosa ajira kutokana na vyuo hivyo kutokuwa na sifa. Rais Magufuli alitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) lenyewe kubaki na udhibiti.

Aidha alisema ni vyema Tume ikabaki na majukumu yake kama kuhimiza ubadilishaji wa maarifa/elimu kwa njia ya kuunganisha kimtandao Vyuo Vikuu na Vyuo vya Vyuo Vikuu, usajili na utambuzi rasmi wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Vyuo Vikuu, uthibitishaji wa programu za kitaaluma, uthibitishaji na uratibu wa udahili wa wanafunzi.

Majukumu mengine ni ufuatiliaji na udhibiti wa elimu bora Vyuo Vikuu na Vyuo vya Vyuo Vikuu, ukusanyaji na usambazaji wa taarifa/ data kuhusu elimu ya juu. “Niombe tu kwa Wizara ya Elimu na TCU tubadilishe kidogo utaratibu wa kuchagulia wanafunzi, wanafunzi wawe wanachagua vyuo badala ya TCU kuwachagulia vyuo vya kwenda,” alisema. Akifafanua zaidi alisema kama wanafunzi wakijichaguliwa vyuo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kingejaa wanafunzi 23,000 wanaotakiwa kuwepo katika chuo hicho.

“Lakini sijajua ni kwa nini mtu amefaulu anataka kuja hapa afaidi mabweni ya Magufuli analazimishwa kwenda kwenye kachuo ambako hakana jina akasome pale, wakati hakuna hata mabweni, saa nyingine hata walimu hawana, tunawatesa watoto hawa,” alisema. Alisema anafahamu ingawa hana ushahidi kuwa wakuu wa vyuo hivyo wanatoa fedha kwa viongozi wa TCU ili wapangiwe idadi ya wanafunzi wanaowahitaji kwenye vyuo vyao.

Rais Magufuli alisema kuwa TCU ibaki kuwa mdhibiti wa elimu lakini wanafunzi wabaki kuwa na haki ya kuchagua vyuo kwani baadhi ya vyuo vinaendesha shughuli zake kwa mikopo ya wanafunzi hao. “Tuwaache watoto wachague vyuo wanavyovitaka, vile ambavyo havitachaguliwa, vife kwanini mnalazimisha vyuo ambavyo havina ubora vipate wanafunzi msipolazimisha vyuo ambavyo vina ubora vitapata watu….. najua maneno haya hayawafurahishi baadhi ya watu na mimi siko hapa kumfurahisha mtu?” alisema Rais Magufuli.

Chanzo: bongo5.com

MKE WA ROMA ATOA YAKE YA MOYONI KUHUSU KUTEKWA KWA MUMEWE.


Mke wa msanii Roma Mkatoliki, Nancy Mshana amefunguka kwa mara ya kwanza toka mume wake alipotekwa na kupatikana na kuwashukuru Watanzania ambao walikuwa pamoja na yeye katika kipindi kigumu.
Roma akiwa na mtoto wake.

Mrembo huyo ametumia maneno ya kwenye Biblia kutoka katika kitabu cha Yeremia kufikisha ujumbe wake kwa watu ambao wamemfanyia ubaya mume wake na kusema kuwa na wao watakutwa na mabaya hayo.

“(Yeremia 30:16-17) Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.Ameen” Alinukuu mke wa Roma Mkatoliki.

Mbali na hilo Nancy alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wote ambao wamesimama na wao katika kipindi hiki kigumu.

“Ahsanteni wote mliosimama na sisi katika kipindi kigumu tulichopitia !! Mungu awabariki sana” aliandika Nancy.

Msanii Roma Mkatoliki bado anaendelea na matibabu kufuatia tukio lake la kutekwa na kuumizwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Alhamisi, 13 Aprili 2017

MWENGE  WA UHURU WIZI MTUPU.

MWENGE wa uhuru umezinduliwa hivi karibuni na Samia Suluhu, Makamu wa Rais katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Morogoro. Mwenge huo “utakimbizwa” nchi nzima.
Mwenge huo kwetu utapita, kwenu umepita au bado? Kama bado basi unakuja. Bahati mbaya tu kwamba kwa mara ya kwanza tangu niwe na akili timamu nilihudhuria mbio za Mwenge mwaka 2011 kwetu Singida.
Niliyoyaona yalinifanya niwalaumu watu wote wakubwa kuliko mimi, ambao kila siku wamevumilia mambo ya hovyo yanayofanywa kwa kivuli cha mbio za Mwenge wa Uhuru.
Ilikuwa ni bahati ya pekee kwa viongozi wa serikali kushindwa kufikiri, hadi wakaamua kunialika nihudhurie katika mbio za Mwenge wa Uhuru. Huko nilijifunza mengi.
Watakaokasirika kwa kusoma haya, wajue lengo langu limefanikiwa, kwani sikuwa na lengo la kuwafurahisha tangu nilipofikiria kuandika haya kuhusu Mwenge.
Upuuzi huu unaanzia katika gharama za kukimbiza Mwenge. Msafara huu unahusisha mkuu wa mkoa, wilaya na sekretarieti zote, usalama wa taifa, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Uhamiaji, Polisi, Jeshi, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi.
Katika hiyo orodha ndefu, watu wote wanalipwa pesa, tangu mkubwa mpaka mdogo, hadi waandishi wa habari. Pesa inayotumika kwa shughuli ya Mwenge ni nyingi. Msafara wa Mwenge unahusisha magari mengi, yanayojazwa mafuta. Magari mengi yenye namba za PT, STK, STL, STJ, RC na magari ya mwenyekiti na katibu wa CCM, pia yapo mengine yenye namba binafsi.
Nikiwa katika Shule ya Msingi Lusilile, ambako yalifanyika mabidhiano kati ya Mkoa wa Singida na Dodoma, niliona takribani magari 120 au zaidi, kwa misafara yote miwili iliyokutana hapo.
Kimsingi, Mwenge unatumia gharama kubwa mno, kiasi kwamba fedha hizo zingetumika kufanya shughuli za maendeleo, baadhi ya kero kwa wananchi ama zingekwisha au kupungua kwa kiasi kikubwa.
Inashangaza kuona kuwa Mwenge ule ulikabidhiwa katika eneo la shule ambayo haikuwa na madawati.
Njia nzima katika Wilaya ya Manyoni, Singida, tangu tumepokea Mwenge, shule zote njiani wanafunzi walikuwa wamejipanga barabarani, hawakusoma siku hiyo. Lakini hata Mwenge haukusimama njiani.
Wananchi wa Lusilile na vijiji jirani waliniambia kuwa kulikuwa na msako maalumu kwa wananchi watakaokiuka kuhudhuria mbio za Mwenge, hivyo walilazimika kujipanga barabarani tangu asubuhi na baadaye kupigwa na jua kali, njaa na kiu zao hadi Mwenge ulipopita.
Wapo waliolazimishwa kucheza ngoma ili ionekane wanaufurahia Mwenge. Kifupi, wapo wananchi ambao hawakufanya kazi za kujiingizia kipato ili kuheshimu amri ya kuhudhuria mbio za Mwenge
Hata hivyo, katika mbio za Mwenge, Mwenyekiti wa CCM na katibu wake, pamoja na viongozi wa Umoja wa vijana wa chama hicho  (UVCCM)  ni watu wa kuheshimiwa kuliko hata askari wa cheo cha juu.
Kuna bajeti ya kuweka mafuta gari ya Mwenyekiti wa CCM, Katibu wa CCM,  wa UWT, na UVCCM, japo wanahadaa kuwa Mwenge ni wa kitaifa. Ni uongo, kuthibitisha hili, huwezi kuona popote risiti ya mafuta kwa magari ya wenyeviti wa mikoa wa TLP, NCCR, CUF, CHADEMA, NLD.
Kichefuchefu kingine ni kwamba kuna fungu la kununua nguo za mapokezi ya Mwenge, zipo tofauti kati ya  ofisi ya mkuu wa mkoa, ofisi ya katibu tawala wa mkoa, ofisi ya mkuu wa wilaya Ofisi ya TAKUKURU, ofisi ya Usalama wa Taifa na viongozi wengine.
Pia unakuta kuna sare za mapokezi ya Mwenge zingine za kimbizia Mwenge.  Fungu la suti hizo zilitosha kununua madawati kwa ajili ya darasa moja la shule waliyoenda kukabidhiana Mwenge ambayo haikuwa na madawati.
Mwenge unatembezwa na kaulimbiu za “kumulika wezi na wala rushwa,” nilishtuka zaidi tulipokuwa Manyoni Mjini, ukarabati wa mnara wa Mwenge, mnara ambao umejengwa miaka mingi huko nyuma, mnara ulipigwa rangi na kuandikwa kaulimbiu ya “Tumethubutu, tumeweza, na Tunasonga mbele” kwa gharama ya Sh. 2.5 milioni. Haiingii akilini. Watanzania tuache kuhalalisha wizi wa kimachomacho kama huu.
Mwenge ni nini? Kwanini unatumika kama alama katika mavazi na kadi za UVCCM? Mwenge una msafara mrefu kuliko hata msafara wa rais?
Katika msafara 


JESHI LA POLISI LATOA TAHADHARI KWENYE MSIMU HUU WA PASAKA.


Jashi la polisi nchini limetoa tahadhari kwa wananchi kuelekea msimu huu wa Sikuu ya Pasaka kuhusiana na suala zima la ulinzi na usalama wa mali zao huku likisema kuwa kuna baadhi ya watu hutumia sikukuu hizi kufanya vitendo vya uhalifu hasa wizi wa kutumia silaha, wizi wa magari, utapeli na vitendo vingine.

Taarifa ndiyo hii hapa chini

RAIS MAGUFULI AMPIGIA SIMU MWANA FA


Jioni ya April 12 2017 staa wa muziki wa hip hop bongo Hamisi Mwinjuma ambaye wengi tunamfahamu kwa jina la Mwana FA, alitoa taarifa kupitia ukurasa wake wa twitter kuoneshwa kufurahisha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kumpigia simu.

Mwana FA ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika radio na tv stations mbambali kwa hit single yake ya Dume Suruali amethibitisha kupigiwa simu na Rais kumwambi anakubali kazi zake.



Kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa staa huyo uliyokuwa verified aliandika “nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais @MagufuliJP kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa #DumeSuruali..”