TUJIKUMBUSHE KIDOGO JUU 2PAC.
Leo Septemba 13 ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyewahi kuwa nyota mkubwa sana kwenye miondoko ya Hip Hop namzungumzia 2pac Shakur a.k.a Makaveli. Ni msanii aliyezaliwa mwaka 1971 East Harlen-New York nchini Marekani na alianza kazi ya muziki mwaka 1987 akiwa kwenye kundi la Digital Underground.
Mbali na kuwa mwanamuziki 2Pac alikuwa ni muigizaji na aliwahi kucheza muvi 6 akiwa kama starring na moja kati ya filamu aliyowahi kutoa ni Gang Related ya mwaka 1993. Hadi mauti yanamkuta 2Pac Shakur alikuwa amewekeza vizuri kwenye albamu maana aliacha albamu 5. Moja kati ya albamu zake ni All eyes on me, Strictly 4 Maniggaz na 7 Day theory (Don Kiluminant).
2Pac Shakur aliwahi kushirikiana na wasanii kama Nate Dogg, Snoop Dog, Rich Richie na The Notorious B.I.G. Amewahi kuwa kwenye kundi la Thug Life na lebo ya Interscope mwaka 1991-1995 kisha lebo ya Death Row mwaka 1995-1996.
2Pac Shakur alifariki dunia majira ya saa 10 jioni Septemba 13 mwaka 1996 ikiwa ni siku 6 tangu kutokea kwa shambulizi lake. Usiku wa tarehe 7 septemba 1996 wakati Pac akitokea kwenye mpambano wa masumbwi kati ya rafiki yake Mike Tyson dhidi ya Bruce Ledon kwenye barabara ya Flamingo ndipo alipovamiwa na watu wasiojulikana wakiwa kwenye gari na kufanikiwa kumchapa risasi 4 na moja kati hizo risasi ilipiga pafu lake la kulia. Baada ya shambulio hilo 2Pac Shakur alikimbizwa kwenye hospitali ya University Medical Centre of Sourthen Nevada ambako ndiko mauti yalimkuta. Mtu aliyefanya shambulio lile hakuwahi kujulikana hadi leo japo kuna watu wengi sana walihusishwa na tukio hilo kama vile hasimu wake wa wakati huo B.I.G na Anderson.
Tutamkumbuka sana 2Pac Shakur kwa uwezo wake mkubwa wa kufanya muziki wa Hip Hop. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu 2Pac mahali pema peponi, Amina.
Imeletwa kwenu na Erasto The Ninja
Tel: 0768801115


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni