UCHAGUZI WA UDOM WAMALIZIKA KWA AMANI.
Na Erasto Julius Ladis.
Yakiwa yamepita masaa kadha tangu majina ya washindi wa nyadhifa mbalimbali kutangazwa ilichukua takribani siku mbili kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma kuweza kupiga kura. Mchakato wa kampeni za nyadhifa mbalimbali za uongozi uliendeshwa ndani ya siku nne huku likishuhudiwa mamia ya wanafunzi waliokuwa wakijitokeza kusikiliza sera za wagombea.
Mnamo tarehe 6 Juni 2018 ndipo zoezi la upigaji kura lilianza katika ndaki zote za elimu zinazopatikana katika chuo hiki kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki na kati. Katika ngazi ya uraisi wa shirikisho (Federal presidential) kulikuwa na wagombea wa pande mbili ambao ni Ndugu Lemma Zahir akiwa na mgombea mwenza Dada Lilian Gabriel wote kutoka ndaki ya Sayansi asilia. Mgombea mwingine alikuwa ni Ndugu Lazaro Roman na Dada Fathia Jombi kama mgombea mwenza.
Pichani ni waliokuwa wagombea uraisi wa UDOM Ndugu Lemma Zahir na Lilian Gabriel.
Katika uchaguzi huu uliofanyika kwa haki na amani, mshindi wa ngazi ya uraisi wa federation alikuwa ni Ndugu Roman Lazaro na makamu wake Fathia Jombi ambaye alipata kura zaidi ya elfu saba akimzidi mpinzani wake kwa takribani kura 2,000.
Pichani ni mshindi wa kiti cha uraisi katika chuo Kikuu cha Dodoma 2018/2019 Ndugu Roman Lazaro na makamu wake Dada Fathia Jombi wote kutoka COES.
TUANGAZIE UCHAGUZI WA KITIVO CHA ELIMU.
Huu ni uchaguzi ambao pia ulishuhudiwa kuwa na upinzani mkali kati ya Ndugu Shampundu Patrick aliyekuwa akichuana vikali na mpinzani wake Ndugu Kwilasa Faustine kutoka BED PPM. Baada ya uchaguzi kumalizika, matokeo yalitangazwa siku ya tarehe 8 Juni mwaka 2018 ambapo mshindi wa uraisi alikuwa ni Ndugu Shampundu Patrick akijinyakulia akiwa na makamu wake Victoria Tembea.
Pichani ni waliokuwa waliokuwa wakiwania ngazi ya uraisi katika ndaki ya elimu (Kushoto ni mshindi Ndugu Shampundu Patrick na pembeni ni aliyekuwa akiwania tiketi hiyo pia Ndugu Kwilasa Faustine)
Wagombea wenza pia wakionesha kuwa uchaguzi haukuwa vita hapo kushoto ni Dada Zawadi na kulia ni makamu wa raisi wa COED Dada Victoria Tembea.
Raisi mteule wa KITIVO cha elimu Ndugu Patrick Shampundu.















