MWANAMKE TAMBUA NI KWANINI KILA MWANAUME HUKU TOSA BAADA YA KUFANYA NAYE MAPENZI.
Na, Erasto Ladis Julius.
Mambo vipi dada zangu? Naamini mko vizuri na mnaendelea salama na majukumu yenu ya kila siku. Wikendi ya leo ningependa nigusie kitu hiki ambacho niliwahi kukiongea kipindi cha nyuma lakini ni bora nikukumbushe uweze kujua vizuri. Kuna wakati unapata mwanaume ambaye unampenda na yeye anakupenda lakini ghafla mahusiano yanaanza kukufifia au kufa kabisa. Sasa leo nakupa sababu ujue ni kwanini hali hiyo hutokea;
1. Kutokujua chaguo lako sahihi.
Hiki ni kitu ambacho wadada wengi mnashindwa kutambua yaani unakuta dada unataka umpate mtu ambaye hakupendi aidha unampenda kwasababu ya mali au pesa alizonazo. Lakini pia unampenda mtu ambaye sio type yako mfano mtu maarufu au mtu wa muonekano mzuri kuliko wewe. Hii itafanya daily uwe mtu wa kutokwa machozi na kuyalaumu mapenzi kumbe tatizo lipo kwako.
2. Msichana kupenda pesa, anasa au vitu vya thamani.
Kuna msemo huvuma mitaani kuwa eti mapenzi ni pesa, yawezekana kweli mapenzi yanaweza kuhusika na pesa lakini kumbuka kuwa mapenzi ya pesa hayadumu. Dada unaweza kumpenda mtu kwasababu ana pesa kumbe yeye nia yake ni kukuchezea kisha kukuacha.
Sambamba na hilo msichana unaweza ukawa na boy ambaye anakupenda lakini pia wewe ukawa unampenda, tatizo litakuja pale wewe utakapotaka kuomba vitu vya thamani kila siku kiasi cha kumchosha hadi akakutosa.
3. Maumbile ya ndani (siri).
Binti unaweza ukawa mzuri sana kwa muonekano wa nje (physical appearance) yaani ukawa na figure nzuri, sura nzuri na kila kitu kizuri ila kuna siri moja nakwambia kuwa kama sehemu zako za siri zitakuwa pana sana basi kila boy atakuwa anachovya na kuondoka.
Utafiti unasema kuwa wanaume wengi hawapendi wanawake wenye maumbile makubwa ya siri kwani hudai kuwa hakuna ladha nzuri waipatayo. Dada ukiona kila mtu anakuacha ebu jichunguze na umuone hata daktari.
4. Tabia chafu.
Mwanzo wa mapenzi kila mtu huficha makucha kutokuonesha tabia zake lakini mambo huja kuwa tofauti pale ambapo mtazoeana. Utakuta msichana ni mpenda wanaume au kwa lugha ya kawaida niseme ni malaya. Tambua kuwa mapenzi ni kuheshimiana na mapenzi yana wivu sana kwa hyo ukiwa ni kiruka njia hakuna mwanaume mwenye moyo wa chuma wa kukuvumilia.
Tabia zingine chafu ni kama kutokuwa na lugha nzuri, kutokuvaa mavazi ya staha na kutokuwa na heshima.
5. Makundi au marafiki.
Kuna wakati boy akawa anakupenda sana lakini kwasababu ya marafiki au makundi mabaya uliyonayo yakamtia wasiwasi bwana wako. Yawezekana boy wako hapendi unywe pombe ila akaona una kundi la wanywa pombe pia boy wako akaona una kundi la watumiaji ambao yeye hawaamini basi tegemea kuachwa.
Kumbuka kuwa marafiki wanaweza kuharibu hata uhusiano wako aidha kwa kukupa maneno ya ajabu kuhusu boy wako au kumtongoza kabisa ili wajue umempendea nini.
6. Wivu na kelele za mara kwa mara.
Mapenzi ya kweli yana wivu lakini wivu ulivuka mipaka huwa ni kero. Wanaume wengi hawapendi kabisa kelele za mara kwa mara na badala yake hupenda mapenzi ya utulivu yenye amani tele. Sio mwanamke kila wakati mara ushike simu ya mwenza wako mara ukiona kasimama na msichana unune, aisee utaambulia mabua.
7. Maringo na usumbufu ukitongozwa.
Kuna wakati mtu akakupenda na kuamua kukufuata ila ukawa una ringa na kumkataa. Mtu huyo huendelea kukomaa na wewe hata baada ya miezi 6 mwisho anakata tamaa sasa siku ukimkubalia na kumvulia nguo hufanya kisha kukutosa. Hii ni kwasababu unakuta umemkubalia muda ambao yeye hakupendi na amekata tamaa na wewe.
8. Hulka ya wavulana wenyewe.
Ukweli kuna wavulana wengine ambao tayari walishakuwa play boys ambao hutamani kila sketi isiwapite. Aina hii ya wanaume huwa na maneno matamu sana na huwa na mbinu nyingi kuwashawishi akina dada na kwasababu akina dada pia ni dhaifu basi hukubali na kuambulia maumivu.
Dada zangu kuna mambo mengi sana ambayo yanafanya uachwe lakini hayo yanakutosha kwa hiyo wajibu ni wako kujipanga kuwania mama bora ila sio kufanywa choo cha kanisa eti kila muumini anaingia.
Mwanamke uchi wako una thamani kubwa zaidi ya elfu 50 ambayo utapewa siku moja. Mwili wako ni lulu ya kuringia kwa watu, kwa hiyo jitambue. Mwili wako ni zaidi ya gari au nyumba kisha uumizwe moyo.
Toa maoni hapa









