LISTI YA WASANII 10 WALIOFANYA VIZURI MWAKA 2017
HII NI LISTI YA WASANII 10 KUTOKA TANZANIA WALIOFANYA POA SANA MWAKA 2017.
Na, Erasto The Ninja.
Yakiwa yamesalia masaa machache sana kuweza kuukamilisha mwaka huu basi ingekuwa ni vizuri zaidi kama ningetaja wasanii 10 bora ambao wameweza kufanya poa sana mwaka 2017. Karibu twende pamoja.
1. ASLAY
Akiwa ni moja kati ya vijana waliotoka kupitia mgongo wa lebel ya Mkubwa na Wanawe kutoka Temeke basi Aslay amekuwa ni moja kati ya vijana ambao wamefanya poa sana mwaka huu. Hakuna wa kupinga kuwa kona zote za mitaa ya hapa nchni Tanzania ulikuwa huwezi kupita bila kusikia wimbo wa Aslay ukichezwa. Akiwa amefanya kazi zake kwa Shirko producer wa Moja Moja Records lakini pia Aslay alifanya hit kali pia kutoka kwa producer Zest. Nyimbo zake kali alizotoa mwaka huu ni kama Natamba, Baby, Pusha na nyimbo kibao tu ambazo siwezi kuzitaja zote.
2. NANDY.
Ni product kutoka Tanzania House of Talent ambapo baadhi ya wasanii kama Barnaba, Amin, Rachel, Beka na Lameck Dotto walipitia hapo. Kuna watu husema kuwa Nandy ndio amekuwa mrithi wa Ruby hasa kwa nyimbo zake kali na jinsi anavyoweza kutumia sauti yake vizuri. Nandy ndiye msanii wa kike ambaye kwa mtazamo wangu ndio kafanya vizuri zaidi mwaka huu.
3. DIAMOND PLATNUMZ.
Kiuhalisia mimi ni Team Kiba ila kwenye kitu kizuri siwezi kusema uongo. Diamond kafanya vizuri sana kwa hit zake alizotoa mwaka huu akiwa pamoja na team yake ya WCB. Diamond amefanya kazi na wasanii wakubwa kama Morgan, Patoranking na The Big Boss *Rick Ross* kutoka USA. Chini ya Producer Laizer jua kuwa Diamond kafanya ngoma kali kama Sikomi, Love you die na ngoma kibao zingine.
4. ALI KIBA.
Ni kijana kutoka Kariakoo Dar es Salaam aliyekuja kutambulika zaidi mwaka 2007 na wimbo wake wa Cinderella aliofanya pale *G. Record* chini ya producer *KGT*. Japo hakuwa na nyimbo nyingi ila hakuna wa kubisha kuwa "Seduce Me" no wimbo wa Kiba ambao ulikuwa gumzo sana nchini Tanzania hasa baada ya kuvunja record ya Vevo Afrika Mashariki. Ali Kiba amepata shoo nyingi sana hasa baada ya kutoa wimbo wa Seduce me uliofanyika kwenye studio za Man Walter (Combination Sound).
5. WEUSI.
Nashindwa nimtaje nani aingie kwenye list hii ila kwasababu wote hufanya kazi kwa ushirikiano basi sina budi kuwaweka hapa. Sio Joh Makini, G. Nako wala Nikki wa Pili ambaye unaweza kutia shaka kwenye kazi aliyoifanya kwenye tasnia ya muziki mwaka huu.
6. VANESSA MDEE.
Moja kati ya wadau ambao husemekana kuwa wana uwezo mkubwa sana wa kutema kimombo basi Vanessa kafanya vizuri sana mwaka huu. Moja kati ya nyimbo alizotoa ni "Mapenzi ya Kisela" akiwa na "Mr. P" wa kundi la "P-Square" kutoka Nigeria. Vanessa Mdee pia kafanya collabo kibao za kimataifa na ndani ya bongo.
7. ZAIID.
Hakuna ngoma iliyopata gumzo bongo kama ngoma ya Zaiid "Wowowo" ambayo imefanya poa sana kwenye vituo vya radio na Tv hapa nchini Tanzania. Zaiid alikuwa kama ni msanii mpya kwenye game la muziki hasa kwa baadhi ya watu lakini ukweli ni kwamba Zaiid ni msanii ambaye alikuwa na nyimbo nyingi tu hata kabla ya wimbo wa "Wowowo".
8. ROSTAM.
Ni kundi ambalo lilianza kama mzaha ila mwisho likawa official. Roma Mkatoliki kutoka Tanga na Stamina kutoka Morogoro ni vijana wawili walioweza kufanya poa sana hasa na wimbo wao wa Hivi ama vile na Kibamia zilizofanyika pale Kiri Record kwa Producer Don.
9. ______________
10. _____________
Nimeacha wazi hapo namba 9 na 10 ili nawewe uweke wasanii wako wawili kukamilisha list hiyo.